Aliyekuwa mwamuzi wa migogoro katika Court of Arbitration for Sport (CAS), Raymond Hack amesema kuwa Senegal inaweza kushinda kesi yao dhidi ya Confederation of African Football kwa sababu uamuzi wa mwamuzi wa mechi ni wa mwisho.

Amesema:“Kanuni ni rahisi sana, mwamuzi ndiye mwenye mamlaka pekee uwanjani na anapopuliza filimbi, huo ndio mwisho wa mchezo. Mambo yote yaliyotokea kabla hayaathiri uamuzi wa mwisho.”

Raymond aliongeza kuwa mwamuzi ndiye mwenye uwezo wa kumaliza mchezo, na katika tukio hilo aliupuliza filimbi mwishoni mwa muda wa nyongeza, ambapo mshindi alikuwa Senegal.

Hivyo, kwa mtazamo wake, Senegal wanabaki kuwa mabingwa wa AFCON 2025.