Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mwanza Alistidia Clemence 

Na Hellen Mtereko,Mwanza

Katika kuhakikisha huduma ya umeme inaendelea kuwa bora Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mkoa wa Mwanza wanaendelea na zoezi la kubadirisha mita zilizokuwa zinatumia rimoti na kuweka Smart meter (Mita janja) ambazo zitasaidia kumrahisishia mteja kufanya manunuzi ya umeme moja kwa moja.

Hayo yamebainishwa Leo Jumatatu Machi 16, 2026 na Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mwanza, Alistidia Clemence alipokuwa akizungumza na Fullshangwe Blog ofisini kwake kuhusiana na maboresho mbalimbali wanayoendelea kuyafanya.

Amesema kumekuwa na changamoto ya wateja kupoteza rimoti,wengine kushindwa kutumia rimoti hivyo uwepo wa Smart Meter utasaidia wateja kujaza umeme kwaurahisi kwani wanaponunua umeme unaingia moja kwa moja.

“Hadi sasa tumeshafunga Smart Meter 1889 na hizi mita tunafunga kwa mtaa kunavifaa ambavyo tunavifunga kwenye transifoma (DCU)tukishafunga tunabadirisha mita za eneo husika na kuzifanya smart miter”,Amesema Clemence

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujiunganishia umeme kinyemela badala yake wafike TANESCO ili waweze kupata elimu na taratibu nzuri za kuunganishiwa huduma hiyo muhimu.

Mwisho ameeleza kuwa zoezi la kubadirisha mita ni bure hivyo wananchi watambue hilo na wasisite kutoa taarifa endapo kunaviashiria vyovyote vya rushwa.

 

 

Mwishooo