Mwandishi wa habari mwandamizi na Mkurugenzi wa Full Shangwe Media, Bw. John Bukuku (kushoto), akiweka shada la maua katika kaburi la mama yake mzazi aliyezikwa Machi 9, 2026, mkoani Songwe.

………..

Mwili wa Marehemu Bi. Anyambilile M. Kilindu, mama wa mwandishi wa habari mwandamizi na Mkurugenzi wa Full Shangwe Media, Bw. John Bukuku, umezikwa Machi 9, 2026 mkoani Songwe katika maziko yaliyohudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki.

Awali, mwili wa marehemu uliagwa Machi 8, 2026 katika ibada iliyofanyika Madale, jijini Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwenda Mbeya kwa ajili ya maziko

Ibada ya kuaga mwili huo ilihudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali waliokusanyika nyumbani kwa Bw. Bukuku kwa ajili ya kuifariji familia na kushiriki kumuaga mpendwa wao.

Baadhi ya waliohudhuria walieleza masikitiko yao kwa kumpoteza marehemu huyo, wakisema katika maisha yake alijulikana kuwa mtu wa Mungu mwenye imani thabiti pamoja na upendo mkubwa kwa watu.

Marehemu Anyambilile M. Kilindu alizaliwa Machi 22, 1930 mkoani Mbeya, na alifariki dunia Machi 7, 2026 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.