Wekundu wa Msimbazi Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ddhi ya B19 FC katika mchezo wa hatua ya 32 CRDB Federation Cup, uliopigwa Machi 7,2026, Uwanja wa Mej. General Isamuhyo.
Watupiaji wa mabao hayo ni Inno Loemba dakika ya 22 kwa pigo la kichwa na Clatous Chama dakika ya 77 akitumia pasi ya Ellie Mpanzu.
Mpanzu na Chama wote walianzia benchi mchezo wa leo. Chama alichukua nafasi ya kiungo Morice Abraham ambaye alianza kikosi cha kwanza.
Matokeo haya yanaifanya Simba SC kutinga hatua ya 16 CRDB Federation Cup ambapo mabingwa watetezi ni Yanga SC.
Mabingwa Yanga SC vs Polisi Tanzania wanatarajiwa kukutana Leo Machi 8 2026 Uwanja wa KMC Complex kutetea taji hilo.
