Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Daniel Sillo, amekabidhi mabati 100 kwa wananchi walioathirika na mafuriko ya mvua katika Kijiji cha Seloto, Kata ya Dareda, leo Machi 5, 2026.
Akikabidhi msaada huo, Sillo ametoa pole kwa wananchi waliokumbwa na janga hilo lililosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali, na kuwataka kuchukua tahadhari zaidi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kipindi hiki cha mvua.
Amesisitiza umuhimu wa wananchi kuwa makini hususan kwa wale wanaoishi maeneo hatarishi ili kulinda maisha yao na mali zao.
Kwa upande wao, wananchi wa Kijiji cha Seloto wameishukuru juhudi za Mbunge wao kwa kuwafikia katika kipindi kigumu walichokumbana nacho, wakisema msaada wa mabati hayo utawasaidia kurekebisha makazi yao yaliyoharibiwa na mafuriko.
