***************************
Na Magreth Mbinga
Wageni wanaoendeleo kuingia Italia lazima wawe na sababu maalumu ya kuzunguka nchini humo.
Kauli hiyo imetolewa na Barozi wa Italia hapa nchini Roberto Mengoni katika mazungumzo yake na waandishi wa habari katika ofisi za ubarozi huo.
Mengoni amesema wiki mbili zilizopita Italia iloathiriwa na ugonjwa wa virusi vya Corona Covid-19 taarifa ya kwanza ilirokodiwa kaskazini mwa Italia mnamo februari 22 na hatua za tahadhali za haraka zimechukuliwa nchini humo.
Pia amesema mpaka jana machi 9 amepokea taarifa ya ongezeko kubwa la maambukizi kati ya watu 9172 watu 7985 ni wagonjwa wa virusi kati yao 724 wamupona na 463 wamekufa.
“Serikali inasoma hatua za kulinda familia na kampuni ambazo zitakabiliwa na shida kubwa imetoa fungu la thamani ya euro billion 7.5 sawa na trilioni 19.6 za Tanzania” amesema Mengoni.
Vilevile Mengoni amesema waziri wa Italia Giuseppe Conte amezindua kampeni ya nakaa nyumbani ni kwadhumuni la kupunguza upanuzi wa virusi kwa watu na kupunguza muingiliano wa kijamii.
“Hii Nishida ya kidunia Kila mtu anaweza kutoa mchango na anaweza kuchukua jukumu la kukabiliana na virusi hivi”amesema Mengoni.
Hata hivyo amemalizia kwa kuzindua ujumbe kwa jamii ya Italia kuwa wapo karibu nao wanawakumbatia wazazi,watoto,jamaa,marafiki,madaktari na wauguzi hospitality,wanasayansi,wafanyabiashara,wanaume na wanawake wa sanaa kwa pamoja wanaweza kushindana kama vile walivyoweza kushinda majanga ya hapo zamani.