Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha Rais wa Jamhuri ya Ghana Mhe. John Mahama wa kwanza (kulia), Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa APCO Worldwide, Bi. Margery Kraus wa pili (kulia) pamoja na Mwanzilishi Mwenza na Mwenyekiti Mtendaji wa GAIS na Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina mara baada ya uzinduzi rasmi wa Jukwaa la Uwekezaji barani Afrika (GAIS), uliofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 03 Februari, 2026
Rais wa Jamhuri ya Ghana Mhe. John Mahama akihutubia viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwekezaji barani Afrika (GAIS), Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 03 Februari, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Angola ambaye pia Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Mhe. João Lourenço kwenye hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwekezaji barani Afrika (GAIS), Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 03 Februari, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa APCO Worldwide, Bi. Margery Kraus kwenye hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwekezaji barani Afrika (GAIS), Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 03 Februari, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwekezaji barani Afrika (GAIS), Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 03 Februari, 2026. Kushoto ni Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina ambaye ni Mwanzilishi Mwenza na Mwenyekiti Mtendaji wa GAIS.
Mwanzilishi Mwenza na Mwenyekiti Mtendaji wa GAIS na Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina akihutubia viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwekezaji barani Afrika (GAIS), Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 03 Februari, 2026.
Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa APCO Worldwide, Bi. Margery Kraus akihutubia viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwekezaji barani Afrika (GAIS), Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 03 Februari, 2026.
Balozi Mstaafu Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield akinyanyua juu glass pamoja na Mwanzilishi Mwenza na Mwenyekiti Mtendaji wa GAIS ambaye pia Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la Uwekezaji barani Afrika (GAIS), Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 03 Februari, 2026.



