Mstahiki Meya wa Ilemela, Sarah Ngh’wani, akizungumza na madiwani (hawapo pichani), leo.

Baadhi ya madiwani wakifuatilia taarifa ya makusanyo ya mapato robo ya pili mwaka wa fedha 2025/26, leo.

Baadhi ya madiwani wakiwa katika kikao cha kupokea taarifa ya mapato ya ndan, robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/26, leo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manspaa ya Ilemel, Dr.Mria Kapinga, leo, akiwasilisha kwa madiwani (hawapo pichani) taarifa ya makusanyo ya mapato ya ndani , robo ya pili ya mwaka waa fedha 2025/26.

Mwenyekiti wa CCM Wlaya ya Ilemela, Yusuf Bujiku , ktoa salamu za Chama katika Baraza la Madiwani wa Manspaa ya Ilemela, leo. (Picha na Baltazar Mashaka)

…………….

Na Baltazar Maashaka, Ilemela

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/26 imekusanya zaidi ya sh. bilioni 7 sawa na asilimia 42.9 ya makisio ya mapato ya ndani ya sh. bilioni 16.45.

Akizungumza leo wakati akiwasilisha taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2025, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Dk. Maria Kapinga, alisema kati ya fedha zilizokusanywa, asilimia 60 zilielekezwa kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema fedha hizo zilitumika zaidi katika sekta za elimu na afya, ambapo kwenye elimu zilielekezwa katika ununuzi wa madawati na ujenzi wa miundombinu ya madarasa kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, huku katika sekta ya afya zikielekezwa kwenye ujenzi wa zahanati za Nyambiti na Nyafula pamoja na kuboresha huduma za upasuaji katika Kituo cha Afya Kayenze.

Aidha, Dk. Kapinga alisema katika kipindi hicho manispaa imetekeleza miradi ya maendeleo yenye thamani ya Sh. bilioni 43.9 kupitia mapato ya ndani, ruzuku ya serikali kuu pamoja na fedha za Mpango wa Uendelezaji Miji na Majiji (UCDG).

Pia, halmashauri imeendelea kutenga asilimia 10 ya mapato yasiyofungwa kwa ajili ya mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ambapo hadi sasa jumla ya Sh. milioni 625 zimekopeshwa kwa vikundi mbalimbali.

Hata hivyo, alisema bado kuna changamoto ya baadhi ya vikundi kutorejesha mikopo hiyo kwa wakati, akivitaka kurejesha ili kutoa fursa kwa vikundi vingine kunufaika, huku vikundi vilivyokidhi masharti vikihimizwa kuomba mikopo kupitia mfumo rasmi baada ya uhakiki wa Idara ya Maendeleo ya Jamii.

Akizungumza katika kikao hicho, Diwani wa Kata ya Buzuruga (CCM), Manusura Said, alisema wananchi wanahitaji maendeleo ya vitendo badala ya maneno, akisisitiza kuwa haiwezekani kutekeleza miradi bila fedha, bado kuna pengo la takribani Sh. bilioni 9 katika ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuwataka wataalamu kuongeza kasi ya ukusanyaji katika miezi mitano iliyobaki ya mwaka wa fedha.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilemela, Yusuf Bujiku, alisema mafanikio yanayoonekana yanatokana na usimamizi mzuri wa Baraza la Madiwani, akibainisha kuwa kero za wananchi zinaendelea kushughulikiwa kwa ushirikiano bila kujali itikadi za vyama, hali inayodhihirisha misingi ya demokrasia na kuonesha kuwa kinachowaunganisha viongozi ni maslahi ya wananchi.

Alisema wananchi wanatarajia kuona kero zao, ikiwemo miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kitangiri, zikishughulikiwa ili waendelee kuiamini CCM na serikali yake inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Wilaya ya Ilemela, Irene Ben Vitta, alipongeza ushirikiano uliopo kati ya madiwani wa CCM na ACT Wazalendo, akisema usawa na mshikamano wao unalenga kuwatumikia wananchi bila ubaguzi wa kisiasa.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela, Mariamu Msengi, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Ali Mkalipa, alisema utekelezaji wa miradi ya maendeleo unahitaji fedha za serikali kuu na mapato ya ndani, hivyo ushiriki wa wataalamu katika ukusanyaji wa mapato ni muhimu ili miradi itekelezwe kwa ubora na kuwanufaisha wananchi.

Alisisitiza umuhimu wa usimamizi wa miradi, kudumisha amani na mshikamano, akiwataka wananchi kuwa mabalozi wa amani kwa kuwa bila amani hakuna maendeleo.

Akizungumza baada ya kikao hicho, Meya wa Manispaa ya Ilemela, Sarah Ngh’wani, aliwataka madiwani, wataalamu na wananchi kudumisha amani na mshikamano ili kuiendesha halmashauri kwa ufanisi, huku wataalamu wakisisitizwa kujikita katika majukumu yao ya msingi.

Aliongeza kuwa, ipo haja ya kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kufikia malengo ya maendeleo na ustawi wa wananchi wa Ilemela.

PICHA

  1. PIC 147-Mstahiki Meya wa Ilemela, Sarah Ngh’wani, akizungumza na madiwani (hawapo pichani), leo.

2.PC 151-Baadhi ya madiwani wakifuatilia taarifa ya makusanyo ya mapato robo ya pili mwaka wa fedha 2025/26, leo.

3.PIC 155- Baadhi ya madiwani wakiwa katika kikao cha kupokea taarifa ya mapato ya ndan, robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/26, leo.

4.PIC 158-Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manspaa ya Ilemel, Dr.Mria Kapinga, leo, akiwasilisha kwa madiwani (hawapo pichani) taarifa ya makusanyo ya mapato ya ndani , robo ya pili ya mwaka waa fedha 2025/26.

5.PIC 165-Mwenyekiti wa CCM Wlaya ya Ilemela, Yusuf Bujiku , ktoa salamu za Chama katika Baraza la Madiwani wa Manspaa ya Ilemela, leo.

Picha na Baltazar Mashaka

Asante

Hide quoted text

On Thu, Jan 29, 2026, 4:21 PM Baltazar Mashaka <[email protected]> wrote:

  1. BILIONI 7 ZAKUSANYWA ILEMELA, MADIWANI WATAKA UWAJIBIKAJI