………
NA DENIS MLOWE IRINGA
MBUNGE wa Iringa Mjini, Fadhili Ngajilo, ameendelea kuonesha dhamira yake ya kuinua michezo katika mkoa wa Iringa kwa kutoa ahadi za maboresho makubwa kwa viwanja mbalimbali ndani ya halmashauri ya Iringa Manispaa.
Akizungumza kwa niaba ya Mbunge Ngajilo, kwenye mkutano wa Maalum wa kujadili michezo uliotishwa na Mkuu wa Mkoa wa Irimga Kheti James, Katibu wa Mbunge huyo, Yahaya Mpelembwa alisema kuwa ofisi ya mbunge kwa kushirikiana na serikali na ushirikiano wake na viongozi wa mitaa na wadau wa michezo, iatahakikisha viwanja vinne muhimu vinakamilishiwa kwa kufanyiwa ukarabati na kuendelezwa ili kuimarisha mazingira ya michezo kwa vijana.
Viwanja Vitakavyofanyiwa Marekebisho na mbunge Ngajilo ni Uwanja wa Shule ya msingi Kihesa ambapo Utasembuliwa (kusafishwa/kuondolewa vikwazo na Utawekewa magoli mapya, Uwanja wa Isakalilo Utasembuliwa utawekewa magoli
Aliongeza kuwa uwanja wa Uwanja wa shule ya msingi Mlandege Utaendelezwa zaidi kwa hatua za kuboresha eneo la kuchezea na miundombinu na uwanja mwingine utakao rekebishwa ni uwanja shule ya msingi Ipogoro utapitiwa upya ili kuangalia namna bora ya kuuendeleza kwa matumizi ya vijana
Aidha, Mbunge alisema kuwa maeneo mengine yaliyotajwa na wananchi, yatachunguzwa ili kubaini uwezekano wa kupata eneo jipya la michezo ambalo linaweza kuendelezwa.
Ngajilo aliwahakikishia wananchi kuwa ataendelea: kuisapoti ligi ya wilaya kusaidia timu mbalimbali za vijana na wanawake kuongesa kuwa atahakikisha anauwaunganisha wadau wa 8 na serikali ili kujenga uhusiano mzuri kwa maendeleo ya michezo.
Aliongeza kuwa ushirikiano kati ya serikali, wadau na wananchi ni muhimu ili michezo iweze kukua na kutoa fursa zaidi kwa vijana.
Kutokana na wingi wa hoja zilizotolewa na wadau , Mbunge Ngajilo alisema kuwa ataendelea kufuatilia mapendekezo yote yaliyojadiliwa na kwamba mazungumzo mengine yataendelezwa katika vikao vijavyo.
