Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akizungumza jambo na Mama Salma Omar Ali Juma (kushoto), Mjane wa Hayati Dkt. Omar Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akifurahia jambo na Mama Regina Lowassa (kulia), Mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wakati alipomtembelea nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 22 Januari, 2026.
Na. Antonia Mbwambo na Veronica Mwafisi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora-Dar es salaam
Tarehe 22 Januari, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewatembelea na kuwajulia hali Mama Salma Omar Ali Juma, mjane wa Hayati Dkt. Omar Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam na Mama Regina Lowassa, mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo Januari 22, 2026.
Mhe. Kikwete amesema, Ofisi ya Rais-UTUMISHI inazingatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuthamini mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu pamoja na wajane wa Viongozi hao Wastaafu ikiwa ni pamoja na kuwatunza kwa mujibu wa Sheria.
Mhe. Rais yupo pamoja nanyi na amenielekeza kufikisha salamu zake kwenu kwa kuwajulia hali, kusikiliza changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi kwa kuwa anathamni mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu pamoja na wenza wa Viongozi hao amesema Mhe. Kikwete
Kwa upande wake, Mama Regina Lowassa, mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemshukuru na kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia ya Hayati Edward Lowassa wakati wote bila kuchoka.
Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa pamoja nasi wakati wote, nitoe shukrani kwa niaba ya familia kwa hekima na busara ambazo mnatumia katika kutuhudumia Wenza wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu,Amesema Mama Lowassa
Aidha, Mama Salma Omar Ali Juma, mjane wa Hayati Dkt. Omar Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemshukuru Mhe. Kikwete kwa kupata nafasi ya kumtembelea na kumjulia hali na kumuomba amfikishie salamu za shukrani Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufuatilia kwa karibu masuala yanayowahusu na kuyatafutia ufumbuzi kupitia Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Mama Salma Omar Ali Juma (wa pili kutoka kulia), Mjane wa Hayati Dkt. Omar Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wengine ni Wakurugenzi na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora.
Mama Regina Lowassa, Mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mama Regina Lowassa (katikati), Mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mama Salma Omar Ali Juma (wa pili kutoka kushoto), Mjane wa Hayati Dkt. Omar Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2026. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Hilda Kabissa na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Dawati la Viongozi wa Kitaifa Wastaafu, Bi. Nyasinde Mukono.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiagana na Mama Regina Lowassa, Mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati alipomtembelea nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 22 Januari, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiagana na Mama Salma Omar Ali Juma, Mjane wa Hayati Dkt. Omar Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati alipomtembelea nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 22 Januari, 2026
Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza na Mama Regina Lowassa Mjane wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2026.
Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Dawati la Viongozi wa Kitaifa Wastaafu, Bi. Nyasinde Mukono (kushoto) akifurahia jambo wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipomtembelea Mama Salma Omar Ali Juma (hayupo pichani), Mjane wa Hayati Dkt. Omar Ali Juma, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.



