Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Asha Rose Migiro akisalimiana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Mafunzo CCM Bw. Kenani Kihongizi huku Banderemo na vifijo vikiawala wakati alipowasili katika ukumbi wa Diamond Jubilee, wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam.
Dkt. Migiro anatarajiwa kuzungumza na mabalozi wa mashina wa wilaya ya Ilala, ambapo atasisitiza mshikamano, uhai wa chama kuanzia ngazi ya mashina na kuimarisha ufanisi wa ujenzi wa CCM kuelekea majukumu ya mbele.

