Mkurugenzi wa Kampuni ya Experian MicroAnalytics ya Ufaransa Bw. Jean Pires leo Alhamisi tarehe 8 Januari, 2026 amefanya ziara katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) zilizopo TAZARA jijini Dar es Salaam. Lengo la ziara hiyo lilikuwa pamoja na mambo mengine kujadili na kubadilishana mawazo na Menejimenti ya Bodi juu ya namna ya kuboresha utoaji huduma kidijiti kwa wateja na wadau wetu wa kimkakati. Menejimenti ya HESLB katika kikao hicho iliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Bill Kiwia.




UGENI KUTOKA UFARANSA WAKUTANA NA MENEJIMENTI YA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI (HESLB)




