……………………………………………………………………………………………..
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
WANAFUNZI wa shule za msingi na sekondari 2,091 mkoani Pwani, kati ya hao wanafunzi 184 walipata mimba na wengine kuacha shule na utoro kwa mwaka 2019 ,idadi ambayo ni kubwa.
Aidha ,wanafunzi 2,221 ambao waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari mkoani humo bado hawajaripoti shule walizopangiwa hadi sasa .
Kufuatia hali hiyo, mkuu wa mkoa wa Pwani’mhandisi Evarist Ndikilo aliwaagiza wakaguzi wa elimu kufanya kazi kwa weledi kwa kufuatilia na kusimamia masuala ya kielimu ikiwa ni pamoja na ufundishaji,mimba,utoro na changamoto za miundombinu.
Akifungua kikao cha wadau wa elimu kujadili hali ya elimu ,kimkoa, Ndikilo alisema, kati ya wanafunzi waliopewa mimba 144 ni wa sekondari na wengine 40 ni wa shule za msingi.
“Hili si jambo la mchezo, mimba hizi ni nyingi ,endapo kila mwaka kuna kuwa na idadi hizi basi baadhi ya watoto wa kike watazima ndoto zao, “:
“:Naomba taarifa za hatua zinazochukuliwa kwa wanaowapa mimba”Katika makabrasha kuna takwimu za mimba lakini wangapi wamechukuliwa hatua hakuna ,inabidi tuwe na utaratibu wa kujua wanaochukuliwa hatua ,”:alisisitiza Ndikilo.
Hata hivyo, alitoa wito kwa wakuu wa wilaya kukaa na wadau wa elimu katika maeneo yao na kupanga mipango madhubuti ya kuboresha elimu kama ilivyo kwa wilaya ya Kibaha kwa kampeni yake ya ELIMISHA KIBAHA ,NJWAYO Education Award na Kisarawe TOKOMEZA ZERO.
Akielezea kuhusu wanafunzi kuripoti shule, aliwataka wanafunzi hao 2,221 wote kuripoti mashuleni hadi ifikapo march 30 mwaka huu.
Ndikilo alifafanua, mzazi ama mlezi atakaepuuza suala hilo achukuliwe hatua za kisheria.
Hata hivyo alisema, ufaulu wa shule za msingi kwa mkoa huo umepanda kwa miaka minne mfululizo ambapo kwa mwaka 2018 mkoa ulikuwa wa 11 na mwaka 2019 umepanda na kuwa mkoa wa 10 kitaifa.
Nae ofisa elimu mkoa wa Pwani,Abdul Maulid alisema ,mwaka jana kulikuwa na changamoto ya wanafunzi 2,091 kuacha shule na utoro ikiwemo mimba 184 ambapo wanafunzi wa sekondari walikuwa 144 na msingi 40.
Tatizo jingine wanafunzi kukosa chakula cha mchana ,kwa kukosa lishe kwa wakati wanafunzi wanadumaa na kushuka kitaaluma.
Maulid alisema kuwa, wanafunzi waliotakiwa kufanya mtihani wa darasa la saba walikuwa 30,000 ambapo 25,685 walifaulu na wanafunzi 24,414 sawa na asilimia 91 ,wamesharipoti shule hadi sasa na 2,221 ndio bado .
“Halmashauri ya Bagamoyo bado wanafunzi 116 hawajaripoti, Chalinze 49, Kibaha 125, Kibaha Mjini 574,Mafia 20,Mkuranga 553,Kibiti 247,Kisarawe 133 na Rufiji wanne.”:alibainisha Maulid.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo alisema Njwayo Education Award imesaidia kuinua taaluma kwa wanafunzi na kufuatilia wanafunzi wenye mimba na kuchukua hatua kwa wanaohusika na mimba hizo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze, Said Zikatimu alisema ,kuna tatizo la upungufu mkubwa wa walimu na maabara lakini kutokana na mkakati waliojiwekea kuinua taaluma maeneo ya pembezoni mwa mji na mjini wamekaa na walimu ili kujadili namna ya kuinua ufaulu.