Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Riziki Pembe Juma, Leo ameshiriki katika matembezi na Bonanza la mazoezi ya viungo, lililoandaliwa na wanamichezo wa Zone “C” na kufanyika katika Kijiji cha Kinduni Mkoa wa Kaskazi Unguja ambapo Mgenirasmi alikuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdullah.
……….
Na Mwandishi Wetu, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Riziki Pembe Juma amewataka Wananchi kujiunga na Vikundi vya mazoezi ili kujenga Afya zao.
Mhe. Riziki ameyasema hayo wakati wa Bonanza la Mazoezi ya viungo katika ap ZONE C, lililofanyika Kituo cha Wajasiriamali Kinduni ambapo Mgenirasmi alikuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Aidha amewaomba wanamichezo kuongeza bidii katika kufanya mazoezi ili kuhamasisha wengine, kupata Ari na morali wa kujiunga na Vikundi hivyo sambamba na kupata Afya nzuri na kujenga upendo miingoni mwao.
Hata hivyo amewataka Wananchi wa Mkoa huo na Zanzibar kwa Ujumla, kuitumia fursa hiyo iliopo kwa kupima afya zao kwani wamerahisishiwa na sio kuifuata maeneo ya mbali.
Mapema akitoa maelezo, Mwenyekiti wa Chama cha Mazoezi ya viungo Zanzibar (ZABESA) ZONE C, Amour Hamad Amour, ametoa wito kwa wanamichezo pamoja na wananchi kujitokeza katika kupima afya zao ili kubaini matatizo walionayo na kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Mgenirasmi katika matembezi hayo, alikuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah ambapo amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dkt Mwinyi, itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha suala la mazoezi linaimarishwa kwa maslahi ya Wananchi.
Mbali na hayo Mhe. Hemed amesema sula la afya ni muhimu na inapotokezea matatizo matibabu ni gharama hivyo amewataka kujiweka sawa ili kuepuka kupata maradhi na kutumia gharama kubwa kwa ajili ya matibabu.




