…………………………………………………………………………………………………..
Na.Queen Alex Meru
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Dkt John Palangyo ametoa msaada wa kitanda Cha kujifungulia katika zahanati ya Samaria iliopo katika kata ya majengo wilayani Arumeru
Mbunge huyo alitoa kitanda hicho jana ambapo kitanda hicho kina thamani ya Laki Tano
Akiongea na wananchi Mara baada ya kukabidhi kitanda hicho Palangyo alisema kuwa miezi minne iliyopita alipewa taarifa kuhusiana na changamoto ya ukosefu wa vitanda katika zahanati hiyo Hali ambayo ilimlazimu Sana kutafuta kitanda hicho
Alifafanua kuwa kupitia msaada huo wa kitanda wanawake wajawazito Sasa wataweza kupatiwa msaada tofauti na hapo awali ambapo mjamzito mmoja tu ndio alikuwa anaweza kupata huduma kutokana na ukosefu wa kitanda
“Hapo awali wanawake wajawazito walikuwa wanateseka naamini kuwa kupitia kitanda hiki kitaweza kuokoa maisha kina mama wengi na bado mimi Kama mbunge wenu Napambana kuhakikisha naendelea kusaidia katika kuimarisha sekta ya afya”aliongeza
Naye mganga mkuu wa zahanati hiyo Miriam Mkwela alisema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati sahihi kwani walikuwa na miaka10 na hawajawai kuwaona viongozi
Alisema kuwa pamoja na hayo bado wao Kama wataalamu wa afya katika zahanati hiyo wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kama zingetatuliwa basi wangeweza kutoa huduma nzuri zaidi.
Miriamu alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa jengo la maabara Hali ambayo inasababisha wagonjwa kuhudumiwa katika mazingira magumu,shimo la kuweka makondo ya wanawake waliojifungua.
Katika hatua nyingine akiongea kwa niaba ya wanawake wa eneo Hilo Jocye Lukumay alisema kuwa hapo awali walikuwa na changamoto ya kitanda wakati wa kujifungua kwani katika zahanati hiyo Kuna kitanda kimoja na ikitokea Kuna wangojwa wawili itabidi mmoja amusubiri mwingine.
“Mjamzito akiletwa wakati wakujifungua na akakuta Kuna mgonjwa mwingine anahudumiwa itabidi amsubiri Hadi amalize hii inatusumbua Sana kwani wanawake wengi wanavunjika moyo kuja na kuamua kujifungua nyumbani” .
Amemshukuru Sana mbunge kwa kuweza kusikia kilio hiko kwani wameteseka kwa muda mrefu kwani watoto wengi wanapotea.