Home Mchanganyiko JESHI LA POLISI LAAHIDI KUONGEZA ULINZI TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA

JESHI LA POLISI LAAHIDI KUONGEZA ULINZI TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA

0

 

Kamishna  wa  Operesheni na mafunzo Jeshi la Polisi  Liberatus  Sabas pamoja na  Mkurugenzi  Mkuu  wa Tume ya Nguvu za Atomiki  nchini  Profesa  Lazaro Busagala wakionyesha hati za Makubaliano  ya  kutoa Ulinzi  na Tume ya Nguvu za Atomik Tanzania jana jijini Arusha

Kamishna  wa  Operesheni na mafunzo Jeshi la Polisi  Liberatus  Sabas akizungumza katika hafla hiyo.

Mkurugenzi  Mkuu  wa Tume ya Nguvu za Atomiki  nchini  Profesa  Lazaro Busagala akizungumza katika hafla hiyo.

…………………………………………………………………………………

Jeshi  la Polisi  nchini  limeingia  Makubaliano  ya  kutoa Ulinzi  na Tume ya Nguvu za Atomik Tanzania, kutokana na eneo hilo kuwa  ni  muhimu  kwa nchi,pamoja na usalama wa nchi  ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa eneo hilo  halitumiwi  na wahalifu.

Akizungumza  wakati wa zoezi hilo jijini Arusha leo Kamishna  wa  Operesheni  Liberatus  Sabas  alisema kuwa  eneo hilo ni muhimu sana kwa usalama wa nchi  hivyo, linahitaji kuwa salama na ulinzi mathubutu ili kuzuia wahalifu kutotumia eneo hilo.

Sabas alisema kuwa ikiwa  ulinzi  hautaimarishwa  katika eneo hilo linaweza kusababisha  vitu vinavyopatika katika eneo hilo la Tume ya Nguvu za Atomiki   kutumiwa vibaya na wahalifu na kupelekea kuleta athari  kwa nchi.

Aidha  alisema  kuwa  ulinzi  wa eneo hilo ni pamoja na kuhakikisha  eneo linakuwa salama ikiwa ni pamoja na  wafanyakazi na nchi kwa ujumla.

“Mkataba  huo  tuliotiliana  saini  sio  mpya  kabisa  ni utaratibu wa kila mwaka kati ya Jeshi la Polisi  na Tume ya Nguvu za Atomiki, ambapo lengo lake ni kuboresha Uhusiano  baina  ya taasisi  hizo  kwa Maslahi Mapana ya nchi.””alisema Sabas.

Kwa  Upande  wake  Mkurugenzi  Mkuu  wa Tume ya Nguvu za Atomiki  nchini  Profesa  Lazaro Busagala   alisema  kutokana na mkataba waliousaini leo  wana matarajio makubwa hasa ya kupanua wigo wa mahusiano  baina   ya tume ya nguvu za atomiki na jeshi la Polisi  kwa  ujumla.

“Kuna maeneo ambayo yanahitaji ulinzi zaidi na maeneo ambayo  yanahitaji  usalama  zaidi hivyo leo tumepanua wigo zaidi na matarajio yetu sasa hivi ni kuhakikisha kuwa Tanzanian inakuwa salama”alisema Profesa Busagala.

Profesa Busagala alisema kuwa makubaliano hayo yameendelea kupanua wigo hivyo taifa litakuwa salama haswa kwa upande  wa mionzi ama nyuklia kuptia ushirikiano na jeshi la hilo la Polisi.