Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Stephen Motambi akifungua mafunzo ya kuzijengea uelewa timu za utekelezaji wa mradi wa PAMOJA yanayofanyika mjini Morogogoro katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Jordan.

Waratibu na wataalam wa utekelezaji wa mradi wa PAMOJA wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Stephen Motambi (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uelewa wa utekelezaji wa mradi huo yanayofanyika mjini Morogogoro katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Jordan.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bw. Josiah Saoke akifafanua jambo kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa PAMOJA, kabla ya Mgeni Rasmi kufungua mafunzo ya kuzijengea uelewa timu za utekelezaji wa mradi wa PAMOJA yanayofanyika mjini Morogogoro katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Jordan.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afya, Ustawi wa Jamiii na Lishe wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bi. Subisya Kabuje, akitoa neno la utangulizi kabla ya Mgeni Rasmi kufungua mafunzo ya kuzijengea uelewa timu za utekelezaji wa mradi wa PAMOJA yanayofanyika mjini Morogogoro katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Jordan.
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Stephen Motambi akiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalam ya utekelezaji wa mradi wa PAMOJA wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, mara baada ya kufungua mafunzo ya kuzijengea uelewa timu za utekelezaji wa mradi wa PAMOJA.

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Stephen Motambi akiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalam ya utekelezaji wa mradi wa PAMOJA wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, mara baada ya kufungua mafunzo ya kuzijengea uelewa timu za utekelezaji wa mradi wa PAMOJA.

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Stephen Motambi akiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa mikoa wa utekelezaji wa mradi wa PAMOJA, mara baada ya kufungua mafunzo ya kuzijengea uelewa timu za utekelezaji wa mradi wa PAMOJA.

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Stephen Motambi akiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka taasisi za kifedha, mara baada ya kufungua mafunzo ya kuzijengea uelewa timu za utekelezaji wa mradi wa PAMOJA.

Waratibu na wataalam wa utekelezaji wa mradi wa PAMOJA wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Stephen Motambi (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uelewa wa utekelezaji wa mradi huo yanayofanyika mjini Morogogoro katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Jordan.
Waratibu na wataalam wa utekelezaji wa mradi wa PAMOJA wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Stephen Motambi (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uelewa wa utekelezaji wa mradi huo yanayofanyika mjini Morogogoro katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Jordan.
…………
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Stephen Motambi amewataka waratibu na watalaam kutoka katika Halmashauri zinazotekeleza Mradi wa kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania Bara (PAMOJA) kwenda kutekeleza kikamilifu mradi huo, ili kutatua changamoto ya umaskini kwa wanawake, kuzuia ukatili wa kijinsia pamoja na kuwahudumia manusura wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Bw. Motambi ametoa wito huo mjini Morogogoro katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Jordan, wakati akifungua mafunzo ya kuzijengea uelewa timu za utekelezaji wa mradi ili ziweze kutekeleza kikamilifu jukumu la kuimarisha fursa za kiuchumi kwa wanawake wa vijijini, kuzuia ukatili pamoja na kutoa huduma kwa manusura wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
“Nendeni mkatekeleze mradi wa PAMOJA kwa ufanisi ili mziwezeshe jamii kuondokana na changamoto za umaskini na ukatili wa kijinsia, itakuwa ni ajabu mpatiwe mafunzo alafu halmashauri zenu zidiwe na halmashauri ambazo waratibu wao hawajapatiwa mafunzo”, Bw. Motambi amesisitiza.
Aidha, Bw. Motambi amewataka waratibu na wataalam hao kuhakikisha wanazingatia mpango kazi ili kufikia malengo ya mradi, ikiwa ni pamoja na kuzingatia muda uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa mradi.
Sanjali na hilo, amewataka waratibu na wataalam hao kujitoa kikamilifu katika kuwasaidia wanawake kujinasua katika lindi la umaskini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyejitoa kutafuta fedha za utekelezaji wa mradi wa PAMOJA ili ziwanufaishe walengwa.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bw. Josiah Saoke amesema waratibu na wataalam hao wanaopatiwa mafunzo wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha jamii wanayoenda kuisimamia inawezeshwa kiuchumi na inaondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekua ni kikwazo kwa wananchi kupiga hatua katika maendeleo.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afya, Ustawi wa Jamiii na Lishe wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bi. Subisya Kabuje, ametoa wito kwa waratibu na wataalam hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa ushirikiano na uadilifu pamoja na kuishirikisha jamii katika kuianisha matatizo yanayowakabili ili kuyapatia ufumbuzi, ikiwemo suala la ubainishaji wa maeneo ambayo vituo vya kulelea watoto mchana vinapaswa kujengwa.
Washiriki wa mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI wanatoka kwenye Mikoa 10 ya Tanzania Bara ikiwemo, Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Singida, Tabora, Rukwa na Arusha, ambapo jumla ya Halmashauri 40 zinanufaika na mradi huo wa PAMOJA kwa kipindi cha miaka 5 (2024/25 hadi 2028/29).



