Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amewataka wakandarasi wote wasiokuwa na uwezo wakufanya kazi katika Mkoa huo kuacha mara moja kuomba kazi katika Mkoa huo kwani kwa sasa watalazimika kufanya kazi Usiku na Mchana kwa msimamizi mkali utakaowekwa lengo ikiwa nikuhakikisha Miradi katika Mkoa huo yote itatekelezwa kama ilivyopangwa.
Mtambi ametoa kauli hiyo Wakati akizungumza na Wananchi wakata ya Isenye Wilayani Serengeti Mkoani mara baada ya kutembelea kukagua kujionea utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa lami sanzate -Natta Km 40 ikiwa nisehemu ya ujenzi wa Barabara hiyo yenye Km 135 mkutano -sanzate -Natta -Ikoma Geti kwa Gharama ya shilingi Billioni 51,788,265,142.75
Akizungumza Meneja wa Tanroads Mkoa wa Mara mhandisi Vedastus Maribe Alisema hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia Asilimia 56 licha ya kukwama kwa Muda lakin sasa Serikali imetoa Takribani Bilion 3 na mkandarasi amerejea eneo la Mradi kuendelea na Kazi
Baadhi ya wanachi wakizungumza wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mara Kwa ufatiliaji katika utekelezaji wa miradi hiyo.




