Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wameibuka na ushindi wa mabao 2–1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa leo, Novemba 8, 2025, kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
JKT Tanzania walikuwa wa kwanza kupata bao kipindi cha pili kabla ya Simba SC kusawazisha na kisha kupata bao la ushindi. Mabao ya Simba SC yalifungwa na Wilson Nangu pamoja na Jonathan Sowah.
Kufuatia ushindi huo, Simba SC imefikisha pointi 9 baada ya kucheza michezo mitatu, huku JKT Tanzania wakibaki na pointi 7 baada ya michezo mitano.



