Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Ndugu Alex Msama, amesema ameona Watanzania wengi wakikosoa au kulaumu kitendo cha Dkt. Tulia Ackson kujiondoa kwenye michuano ya kugombea Uspika wa Bunge kwamba labda kuna kitu kibaya, au hatakiwi, au amesusa.
Msama amesema kujitoa kwa Dkt. Tulia ni jambo zuri linaloashiria ukomavu wake wa kiuongozi na kidemokrasia. Amesema Dkt. Tulia hana kashfa mbaya, siyo fisadi, siyo mla rushwa, bali ameonesha kwa vitendo ubora wake katika uongozi hadi kuchaguliwa kuwa Rais wa Wabunge wote Duniani.
“Amewaachia nafasi wengine waweze kupata baada ya yeye kufanya vizuri katika kipindi chake, inaonesha hana tamaa ya madaraka, na kwa uwezo wake mkubwa ni matumaini yangu kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atamteua katika nafasi nyingine kubwa ili aendelee kuwatumikia Watanzania,” amesema Msama.



