Na Silivia Amandius.
Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera ameungana na wananchi wa mkoa huo kutimiza wajibu wao wa kikatiba wa kupiga kura, akiwahimiza kufanya hivyo kwa amani na utulivu. Mkuu huyo wa mkoa aliwasili katika kituo cha kupigia kura akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima, na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Jacob Nkwela.
Amesema maandalizi yote ya Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) yako katika hali nzuri, na vifaa vya kupigia kura vimegawanywa kwa wakati katika vituo vyote vya mkoa huo. Alisisitiza kuwa serikali imejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa uwazi na ufanisi ili wananchi waweze kuchagua viongozi wanaowataka.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amewahakikishia wananchi usalama wa kutosha katika maeneo yote ya kupigia kura na kuwataka wajitokeze kwa wingi bila woga, akisisitiza kuwa utulivu na amani ni nguzo muhimu katika kulinda demokrasia na maendeleo ya taifa.




