Mgombea wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan. 
NA JOHN BUKUKU – MWANZA
Kadri siku ya kupiga kura inavyokaribia, Watanzania wengi hasa wa mikoa ya kanda ya ziwa wameendelea kueleza imani yao kubwa kwa Mgombea wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakisema ameonesha mfano wa uongozi unaojali watu na unaolenga kujenga uchumi unaowagusa wananchi wote, bila kujali nafasi zao za kijamii.
Katika kipindi chake cha uongozi cha miaka minne, Dkt. Samia ameweka mkazo katika utekelezaji wa miradi ya kiutu – miradi inayobadilisha maisha ya wananchi mmoja mmoja, vikundi vya kijamii, na taasisi mbalimbali – sambamba na kusimamia miradi mikubwa ya kimkakati kama reli ya kisasa (SGR), bwawa la umeme la Julius Nyerere (JNHPP), barabara, madaraja, bandari na uboreshaji wa huduma za kijamii.
TRENI YA UMEME (SGR)
Lakini tofauti na kipindi kingine chochote, miradi hiyo haijabaki kuwa takwimu kwenye makabrasha ya serikali; imekuwa chanzo cha fursa kwa maelfu ya Watanzania.
Vijana wamepata ajira, wanawake wamewezeshwa kupitia mikopo midogo, wajasiriamali wamepata masoko mapya, na taasisi binafsi zimepata nafasi ya kushiriki katika utekelezaji wa miradi hiyo.
DARAJA LA JPM
Kwa mujibu wa wananchi waliozungumza na Fullshangweblog jijini Mwanza, mafanikio hayo yameleta mabadiliko ya kweli katika maisha yao ya kila siku.
“Tumeona shule mpya zikijengwa, vituo vya afya vikiboreshwa, na hata barabara za vijijini kufunguka. Haya yote yamechochea biashara ndogo ndogo na kuleta ajira nyingi. Huyu ni kiongozi wa watu,” alisema Bi. Zainabu Shabani, mkazi wa Igoma.
VITUO VYA AFYA
“Sasa vijana wengi wameanza kujiajiri kupitia fursa za miradi ya serikali. Dkt. Samia hakubaki na mipango ya karatasi bali amewafanya Watanzania washiriki kwenye uchumi,” aliongeza Bw. Joseph Mtemi, kijana mjasiriamali wa Nyegezi.
Kwa upande wake, wachambuzi wa masuala ya kiuchumi wanasema Dkt. Samia amefanikiwa kugeuza dhana ya maendeleo kuwa jumuishi zaidi. Kila sekta – kuanzia kilimo, uvuvi, viwanda, afya, elimu hadi fedha – imepewa kipaumbele cha kuleta matokeo yanayomgusa mwananchi wa kawaida.
WAJASIRIAMALI
Kupitia miradi kama ya TASAF, mikopo ya Halmashauri kwa wanawake na vijana, na uwezeshaji wa wajasiriamali wadogo, serikali yake imejenga mfumo wa uchumi unaowapa watu uwezo wa kushiriki moja kwa moja kwenye mnyororo wa uzalishaji na uboreshaji wa kipato.
Hali hii imefanya wananchi wengi kuamini kuwa Dkt. Samia anastahili kuendelea kuiongoza Tanzania, kwani amedhihirisha kuwa maendeleo si tu kujenga miundombinu, bali ni kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na matokeo ya uwekezaji wa serikali.
KILIMO CHA UMWAGILIAJI
“Tumwunge mkono Dkt. Samia. Ni kiongozi anayetengeneza fursa za kweli za kiuchumi. Kura yetu kwake ni kura ya maendeleo yenye kugusa maisha ya watu,” alisema Mwalimu Festo Mgaya wa Wilaya ya Ilemela.
Zikiwa zimesalia siku mbili tu kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025, wito unatolewa kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba kwa amani na utulivu, na kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuijenga Tanzania yenye uchumi jumuishi na maendeleo kwa wote.
“Dkt. Samia ameweka msingi wa maendeleo ya kiutu – ni jukumu letu kuhakikisha anapewa nafasi ya kuendeleza kazi njema aliyoianza.”
BARABARA ZA LAMI KUUNGANISHA MIKOA NA WILAYA

BARABARA ZA VIJIJINI NA MADARAJA

MAJENGO YA SHULE

BWAWA LA KUFUA UMEME LA NYERERE



