Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na ujumbe wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACEOM) Ikulu, Zanzibar.
Misheni hiyo inayoongozwa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Uganda, Mhe. Dkt. Specioza Kazibwe imejipanga kufanya uangalizi katika mikoa tisa ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Wakiwa nchini wameweza pia kukutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi ikiwa ni sehemu ya majukumu yao.




