Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha-Rose Migiro, amekutana na Mhe. Mokgweetsi Eric Kaebetswe Masisi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Botswana na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika (AU). Mazungumzo yao yamehusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Jopo la Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika lipo nchini kufuatilia hatua za maandalizi ya uchaguzi huu wa saba tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi miongo mitatu iliyopita.




