Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro leo Alhamis tarehe 16 Oktoba 2025, amewasili mkoani Katavi, akitokea Mkoa wa Kagera, kwa ajili ya kuendelea na kampeni za kumnadi Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan na wagombea ubunge na udiwani wa CCM.
Mapokezi ya Balozi Dkt. Migiro mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Mpanda, yaliongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Kayanza Pinda na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Ndugu Iddi Kimanta.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kqa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwasili mkoani Katavi kuendelea na kampeni za kuomba kura za wananchi wa mkoa huo, pia kuinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025 – 2025, kuwanadi wagombea ubunge na madiwani, baada ya kumaliza Mkoa wa Kagera.