Mgombea Ubunge wa Jimbo la Karagwe ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Innocent Bashungwa, amewaalika Wananchi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya za Karagwe na Kyerwa kuhudhuria mkutano wa kampeni za Mgombea Urais wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, utakaofanyika kesho tarehe 15 Oktoba 2025 katika uwanja wa Bashungwa – Kayanga.
Bashungwa ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera kujitokeza kwa wingi kumpokea Dkt. Samia na kuonesha umoja, upendo na imani, akisisitiza kuwa katika uongozi wake Rais Samia ameleta mafanikio makubwa ya maendeleo katika sekta mbalimbali nchini
“Nitumie nafasi hii kuwakaribisha muungane nasi kumkaribisha Rais wetu Dkt. Samia. Tumuoneshe upendo, shukrani na mapenzi yetu, kwani Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa sana hapa Karagwe na katika mkoa wetu wa Kagera,” amesema Bashungwa
Aidha, Bashungwa amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Kagera kujitokeza katika maeneo yao kulingana na ratiba ya kampeni, ambapo Dkt. Samia anatarajiwa kufanya mikutano ya hadhara tarehe 15 hadi 16 Oktoba 2025 katika majimbo mbalimbali ya mkoa huo.