Mama Janeth Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu kundi la Vijana Jesca Magufuli
……….
NA JOHN BUKUKU ,GEITA
MJANE wa Rais wa awamu ya Tano Janeth Magufuli amemtakia kila laheri Mgombea Urais wa wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumuombea kwenye safari yake ya Urais huku akieleza kwamba atakuwa mstari wa mbele Ockoba 29 kumuombea kura kwa wana Chato na Geita kwa ujumla.
Kauli ya Janeth imetolewa kwa niaba yake na Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu kundi la Vijana Jesca Magufuli wakati akitoa salamu za Mama yake katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kupitia CCM uliofanyika Bukombe mkoani Geita.
Akizungumza katika mkutano huo Jesca alimueleza Dkt. Samia kwamba mama yake alitamani angekuwepo katika mkutano huo lakini kutokana na changamoto ameshindwa kuhudhuria na hivyo amenituma anakutakia kila laheri na anakumbea safari yako ya Urais na atakuwa mstari wa mbele Octba 20 kukuombea kura kwa wana Chato na Geita wote.
“Ndugu zangu nimepewa dakika chache za kuongea naitwa Jesca Magufuli mgombea ubunge kupitia viti maalumu lakini kupitia Kundi la Vijana nimesimama kwa heshima kubwa kukuombea kura Mwenyekiti wetu na mgombea Urais”Alisema
Alisema kwamba mwenye macho hambiwi tazama kutokana na mambo makubwa ya kimaendeleo yaliyofanywa na Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni mchapakazi,Jasiri na mwenye maono mapana na makubwa kwa Taifa la Tanzania.
Jesca alisema kwamba Dkt. Samia alichukua kiti cha Urais kutoka kwa mtangulizi wake hayati John Magufuli lakini kwa miaka minne ameweza kufanya na kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati aliyoanzishwa na mtangulizi wake pamoja na kuanzisha mengine mipya.
Alisema kwamba na miradi mingi inajieleza yenyewe ukianza na mradi wa SGR leo Dar kwenda Dodoma unatumia masaa matatu huku akieleza pia Mgombea Urais huyo amewezea kukamilisha ujenzi wa Daraja la Kigongo Busisi na Bwawa la Mwalimu Nyerere jambo ambalo ni hatua kubwa kimaendeleo.