Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wake mdogo wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Kakonko,leo Oktoba 12, 2025 mkoani Kigoma.
Katika mkutano huo,Dkt.Nchimbi pamoja na kunadi Sera na Ilani ya CCM ya 2025-2030,pia alimuombea kura za ushindi wa kishindo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.
Pamoja na mambo mengine,Dkt Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi baadhi ya wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Kakonko, Ndugu Alan Thomas Mvano pamoja na Madiwani.
Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 22 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.