NA JOHN BUKUKU- MUSOMA
“Niwaambie jambo moja kwamba katika uendeshaji wa nchi hakuna majaribio. Nchi hupewa yule ambaye unamuamini ataendesha vyema na kuhakikisha maslahi ya wananchi yanapatikana,” amesema Dkt. Samia.
Dkt. Samia amesema kuwa maendeleo na maslahi ya wananchi yanatokana na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi pekee. “Msicheze na jambo hili, msidanganyike, kura zenu zitaamua safari ya maendeleo iendelee,” amesema Dkt. Samia.
Aidha, Dkt. Samia amesema, “Ninapowaambia kuwa nimeamua kuanza na wilaya hii ya Bunda, mapokezi ndani ya mkoa wa Bunda yameonesha dalili njema. Asanteni sana kwa kujitokeza kwa wingi, hii inaonyesha imani kubwa kwa chama chenu na wagombea wenu. Niwaombe imani hii iendelee hadi tarehe 29, kwenye vituo vya kupigia kura.”
Aidha, amewashukuru viongozi wa mkoa na wilaya pamoja na wananchi wa Bunda kwa maandalizi mazuri na ushirikiano. Dkt. Samia amesema kuwa wilaya ya Bunda imepiga hatua kubwa kwenye maendeleo, ikiwemo sekta ya afya, maji, elimu na umeme.
“Tumetengeneza miundombinu ya afya katika hospitali za wilaya, tumeongeza upatikanaji wa dawa na vifaa. Kwenye elimu, sasa tumefikia asilimia 95. Katika maji, tumeendelea kutoa huduma kwa wananchi wote,” amesema Dkt. Samia.
Aidha, Dkt. Samia amebainisha kuwa maendeleo ya kiuchumi ni muhimu. “Tumeweka nguvu kwenye kilimo, uvuvi, ufugaji na barabara.
Kwa kilimo, tumejenga skimu za kumwagilia ili wakulima walime mara mbili kwa mwaka na tumeongeza pembejeo za ruzuku.