Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akipokelewa na wakazi wa kata ya Muzye jimbo la Kasulu vijijini waliolazimika kumsubiri hadi usiku ili apite kuwasalimu katika eneo hilo mkoani Kigoma, Oktoba 07, 2025. Zitto yupo mkoa wa Kigoma akiwanadi wagombea wa udiwani na ubunge wa chama hicho ambapo leo, alikuwa katika jimbo la Kasulu vijijini kumnadi, Bigaye Enock anayegombea jimbo hilo
……….
Chama cha ACT Wazalendo kimeahidi kufanya kampeni kwenye kila kona ya nchi endapo mahakama kuu itatoa maamuzi yatakayoruhusu Luhaga Mpina kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho.
Mnamo septemba 15, 2025 Mwanasheria mkuu wa serikali, Johari Hamza alimwekeza pigamizi mgombea huyo lililopelekea kuondolea kwenye kinyang’anyiro cha mbio za Urais na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Kauli hiyo imetolewa jana, Oktoba 06, 2025 na kiongozi mstaafu wa cham hicho, Zitto Kabwe wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Katanga jimbo la Kakonko mkoani Kigoma alipokiwa akimnadi mgombea ubunge wa chama hicho katika jimbo hilo, Olaf Kaboboye.
“Hata kama ikibaki wiki moja ya kampeni tukiruhusiwa tu kugombea, tukishinda mahakamani tutapiga jaramba kila kona ya nchi hii na tutashinda na kuing’oa CCM madarakani” , alisema Zitto
Aliongozea pia endapo chama hicho hakitashinda mahakamani kitatoa maelekezo kwa wananchi namna watakavyopiga kura nafasi ya Rais .