Kamishna wa Polisi Jamii, CP Faustine Shilogile, Oktoba 06, 2025 amepata fursa ya kumtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Gosheni Safaris, Peter Robert, Kampuni inayojihusisha na masuala ya Utalii hapa nchini.
Kamishna Shilogile alimtembelea Ofisini kwake Jijini Arusha mahsusi kumshukuru kwa namna anavyojitoa katika kutoa misaada mbalimbali ikiwemo matengenezo ya magari na misaada mingine mingi ambayo imekua ni chachu katika kupunguza uhalifu.
Kwa upande wake Peter Robert ameshukuru Jeshi la Polisi kwa kuthamini anachokifanya na ameahidi kujitoa zaidi kutoa misaada ya hali na mali pale atakapokua amejaaliwa kwa lengo la kuhakikisha usalama wa WATALII na nchi kwa ujumla.
Kamishna Shilogile aliambatana na Mkuu wa Ushirikishwaji wa Jamii, Naibu Kamishna, Henry Mwaibambe pamoja na Polisi Kata wa Kata ya Ikoma, Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara Sajenti Emmanuel Kisiri ambaye amekua mstari wa mbele katika kushirikiana na wadau mbambali katika kuzuia uhalifu zaidi upande wa UTALII.