Mgombea ubunge Jimbo la Nkasi kaskazini Salum Kazukamwe wakati akinadi sera za chama cha mapinduzi CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kitongoji cha Ntanga kijiji cha Mandakerenge kata ya Kipili
Mgombea udiwani kata ya Kipili Elias Sambwe Meneja wakati akinadi sera za chama cha mapinduzi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Mandakerenge
……….
Na Neema Mtuka , Nkasi
Rukwa : Mgombea ubunge Jimbo la Nkasi kaskazini Salum Kazukamwe amewaahidi wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kuwawekea umeme na kuwasogezea miundombinu ya shule itakayo wawezesha wanafunzi kusoma bila changamoto.
Amesema akipata ridhaa atahakikisha anaondoa changamoto ya ukosefu wa shule pamoja na miundombinu ya barabara itakayo wasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya usafiri.
“Nikipata ridhaa nitahakikisha ninaweka msukumo mkubwa kwenye umeme ili kila mwananchi aweze kuhifadhi samaki katika vyombo vya kuhifadhia samaki kwa kuwa shughuli kubwa ya wakazi hao ni uvuvi amesema Kazukamwe.
Amesema hayo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kitongoji cha Ntanga kijiji cha Mandakerenge kata ya Kipili Jimbo la Nkasi kaskazini.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mandakerenge akiwemo magreth Nzyungu amesema kupatikana kwa shule kutapunguza mimba na ndoa za utotoni.
Akizungumza leo Oktoba 6 ,2025 mkazi wa kata ya Kipili Rafael Fataki amesema wanafunzi walikuwa wakitembea umbali mrefu wa kilomita 20 kwenda shule jambo lililokuwa likihatarisha maisha yao
“Kutokana na hali hiyo ya kutembea umbali mrefu wanafunzi wengi walikata tamaa na kushindwa kumaliza masomo yao.”amesema Fataki.
Amesema kama shule itapatikana itapunguza utoro kwa wanafunzi na kutawasaidia wanafunzi kusoma kwa bidii na katika mazingira mazuri.
Mgombea udiwani wa kata hiyo ya Kipili Elias Sambwe Meneja amesema akipata ridhaa na kuwa diwani wa kata hiyo atashiriakiana na mbunge kukamilisha ujenzi wa shule ambayo ulianza kwa nguvu za wananchi.
Kukamilika kwa mradi huo kutapunguza mimba,utoro na kuchelewa kwa wanafunzi ambao walikuwa wakisoma Kijiji cha jirani kwa kuvuka ziwa Tanganyika.
Kijiji hicho kina jumla ya watoto 250 kati yao wasichana ni 150 na wavulani ni 100 na wanafundishwa na mwalimu mmoja anayejitolea kwa kulipwa na wazazi wa watoto hao.