MWANZA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Balozi Asha-Rose Migiro leo, tarehe 06 Oktoba 2025, ameongoza kikao kazi kwa njia ya mtandao na Makatibu wa CCM Nchi nzima.
Aidha kikao hicho Katibu Mkuu amezungumza na Makatibu wa CCM Mikoa yote nchini kwa lengo la kufahamu mwenendo ulivyo kuelekea Uchaguzi Mkuu 29 Oktoba,2025. Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza zilizopo Kata ya Nyamagana.