Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewasili mkoani Tabora leo Oktoba 4, 2025 tayari kwa kufanya mikutano ya kampeni.
DK Nchimbi anaingia katika mkoa wa 18 kufanya kampeni ya kumuombea kura Mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan, kuombea kura wagombea ubunge na udiwani wa CCM pamoja na kunadi Ilani ya chama hicho ya mwaka 2025 – 2030