Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiwa na Mkurugenzi uzalishaji wa kampuni ya maziwa ya Asas, Ahmed Abri na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakijaribu moja ya bajaji 40 ambazo zimetolewa kwa mkopo kwa Umoja wa madereva bajaji mkoa wa Iringa (UMBI) na kudhaminiwa na kampuni ya maziwa ASAS
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akikata utepe kuzindua uandikishwaji wa madereva bajaji kuweza kukata bima ya afya ambapo wamedhaminiwa na kampuni ya maziwa ya Asas ambapo mkurugenzi wake Ahmed Salim Abri akiwa pembeni mwa kushoto kwal Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimkabidhi cheti cha Shukrani Mkurugenzi uzalishaji wa kampuni ya maziwa ya Asas, Ahmed Abri mara baada ya kukabidhi bajaji 40 kwa kikundi cha umoja wa madereva bajaji mkoa wa Iringa (Picha na Denis Mlowe).
*****************************
NA DENIS MLOWE,IRINGA
KAMPUNI ya Asas Group ya mjini Iringa imekidhamini kikundi cha Umoja wa Madereva Bajaji Iringa (UMBI) na kufanikiwa kupata mkopo wa bajaji 40 zenye thamani ya Milioni 280 kwa lengo la kukopeshana na kurudisha ndani ya mwaka mmoja.
Mkopo huo uliotolewa na Finca Microfinance Bank umekabidhiwa juzi na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi mbele ya mlezi wa kikundi hicho, Mkurugenzi Uzalishaji wa Maziwa ya Asas,Ahmed Salim Abri ikiwa ni udhamini wa kampuni hiyo kulipwa na wanufaika wa bajaji hizo katika kipindi cha miezi 12 kuanzia sasa kwa kupitia umoja wao huo.
Licha ya udhamini huo Mkurugenzi huyo, amewawezesha udhamini, amewaahidi kuchangia kiasi cha sh. 50,000 kwa madereva bajaji 100 kwa ajili ya kuwakatia leseni na wao kuongeza 20,000 kati 70000 zinazohitajika katika ukataji wa leseni na kuwakatia bima ya afya.
Akizungumza kabla ya kukabidhi bajaji hizo, Ahmed Salim Abri alisema awali aliwataka madereva hao kupeleka majina ya madereva 100 kwa ajili ya kuwalipia leseni lakini madereva hao walishindwa hivyo wakati huu amewasisitiza zaidi kufikisha majina hayo aweze kuwaongezea gharama za leseni ni Sh 70,000 na kutoa 50000 na madereva hao kuchangia 20,000 ili aweze kupata leseni.
Alisema kuwa licha ya kuwasaidia madereva hao, ameweza kuwadhamini chama cha walemavu mkoa wa Iringa kupata bajaji 1 na kutoa milioni 1 za kuwadhamini na kufanikisha upatikanaji wa bajaji hiyo kwa ajili kufanya biashara na kuongeza kipato kwa chama hicho.
Aidha aliwapongeza madereva hao na akawataka wazingatie sheria zote muhimu zikiwemo za barabarani wakati wakitumia vyombo hivyo kuepuka mgongano na kikosi cha usalama barabarani.
Akikabidhi bajaj hizo, Waziri Lukuvi aliipongeza kampuni ya Asas kwa udhamini wake kwa madereva hao na kumpongeza Ahmed Abri kwa kuweza kuwasaidia vijana katika changamoto ya ajira kwa kupitia biashara ya bajaji na kuwafanya kuweza kujitegemea lakini pia kuendana na falsafa ya Rais Dk John Magufuli ya Hapa Kazi Tu.
Aidha Lukuvi alitoa wito kwa mkurugenzi huyo kuwaangalia madereva bajaji wa jimbo la Ismani na kuwawezesha kupata mkopo wa bajaji ambapo alisema kwamba bajaji zaidi zinahitajika kuweza kuwakopesha hadi kufikia idadi ya bajaji 100.
Awali mwenyekiti wa UMBI Norberth Sunka alisema tangu kuanzishwa kwa umoja wao miaka mitatu iliyopita wamekwishapata mikopo ya zaidi ya Sh Milioni 670 zilizowawezesha kupata bajaj zaidi ya 95 na kuzikopeshwa kwa wanachama wake.
Alisema kuwa walianza na mkopo wa bajaji 9 ambazo walikupoeshana wanachama wa UMBI kwa gharama ya milioni 50 ambapo walifanikiwa kulipa kwa wakati na kwa kupitia udhamini wa kampuni hiyo wamekwisha kupeshwa bajaji 97 ambazo zimewakomboa kuondokana na kuajiliwa.
Sumka alisema Wanachama 40 ambao awali walikuwa madereva wa bajaji za watu wengine wamenufaika na mkopo huo na kuwawezesha kumiliki bajaji zao wenyewe kutokana umoja wao ambao umekuwa wepesi kulipa mikopo hiyo ndani ya wakati.