Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Muheza katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM mkoani Tanga tarehe 29 Septemba, 2025.
Wananchi wa Muheza wamekuwa na shauku. kubwa kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ambaye alishangiliwa wakati wote wa hotuba yake wakati akizungumza na kuomba kupigiwa kura za ndiyo katika uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika nchini kote
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muheza Ndugu Hamis Mwijuma ‘Mwana FA’ mara baada ya kuwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Muheza mkoani Tanga tarehe 29 Septemba, 2025.
Matukio mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Muheza mkoani Tanga tarehe 29 Septemba, 2025.
Sehemu ya wananchi wa Muheza mkoani Tanga waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) tarehe 29 Septemba, 2025.