Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha-Rose Migiro, akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Sabasaba, Kibaha mkoani Pwani, Septemba 28, 2025.
…………
Tayari Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amewasili na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa chama na wa dini pamoja na maelfu ya wananchi wa Kibaha, mkoani Pwani, katika viwanja vya Sabasaba kwa Mbonde. Wananchi walijitokeza kwa wingi wakiwa tayari kumlaki na kumsikiliza Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, anayetarajiwa kunadi sera na ahadi za CCM pamoja na kuomba kura za “Ndiyo” kwa mafiga yote matatu (Rais, Wabunge na Madiwani) leo, Septemba 28, 2025.
Pamoja na hayo, wananchi wa Kibaha wametuma salamu zao za upendo kwa Rais Dkt. Samia, ambazo wamemuomba Katibu Mkuu Dkt. Migiro kuziwasilisha kwake.
Huu ni muendelezo wa mikutano ya kampeni za urais kupitia CCM, na sasa ni zamu ya Mkoa wa Pwani.