PICHA mbalimbali za matukio ya Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi za mkutano wake wa hadhara wa Kampeni uliofanyika katika uwanja wa Isele, Ilula wilaya ya Kilolo mkoani Iringa,leo Alhamis Septemba 25,2025.
Dkt.Nchimbi ameendelea kupasua anga kusaka Kura za ushindi wa kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.
Pamoja na kuwahutubia Wanachi katika mkutano huo,Dkt.Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kilolo,Ndugu Ritta Kabati ,Wagombea Ubunge wa mkoa huo pamoja na Madiwani.
Dkt. Nchimbi anaendelea kunadi sera na Ilani ya CCM ya mwaka 2025 – 2030 sambamba na kusaka kura za ushindi wa kishindo za Mgombea urais wa chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani