NA JOHN BUKUKU – MCHINGA, LINDI
Mbunge mstaafu wa Jimbo la Mchinga, Mudhihir Mudhihir, amesema maendeleo mbalimbali yaliyofanikishwa katika jimbo hilo chini ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yamechangia kubadilisha maisha ya wananchi.
Ameyasema hayo Septemba 25, 2025, katika mahojiano maalum na Fullshangweblog Kando ya mkutano wa hadhara wa kampeni ukiofanyika Nchinga , ambapo alimpongeza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Mgombea Ubunge wa Jimbo la M lovechinga, Salma Kikwete, kwa juhudi zao za kuendeleza wananchi na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“Salma Kikwete angeweza kupumzika nyumbani, lakini amekuja kuchukua shida za wananchi ili awape raha zake. Kuna fursa nyingi hapa kama korosho, ufuta na samaki. Tukiamua kuzitumia, zitaleta ajira na kuongeza kipato cha wananchi,” alisema Mudhihir.
Aidha, alibainisha kuwa mpango wa kuanzishwa kwa kongani ya viwanda Mchinga utakuwa chachu ya ajira kwa vijana, ikiwemo viwanda vya kuchakata samaki na mbegu za ufuta kuwa mafuta.
Vilevile, alisema jitihada kubwa zimefanyika katika sekta ya afya, ikiwemo kuanzishwa kwa zahanati na vituo vya afya katika vijiji vilivyokuwa havina huduma hizo.
Kadhalika, alieleza kuwa vijiji vyote vya jimbo vimeunganishwa na umeme, isipokuwa vitongoji 32 kati ya 47 ambavyo bado vinaendelea kuunganishwa.
Kwa upande mwingine, alibainisha changamoto ya wanafunzi kuvuka bahari imepatiwa suluhu baada ya kujengwa daraja la miguu ambalo pia hutumiwa na watu wazima na bodaboda.
“Kwa kweli hatuwezi kuhesabu, mama amefanya kazi kubwa sana. Ndiyo maana wananchi wanasema, ukisema Salma, acha mwenyewe,” alisema Mudhihir.
Aidha, alisema kuwa Salma Kikwete anahimiza mshikamano kwa wananchi wa Nchinga bila kujali tofauti za kisiasa. “Kuna wana CCM, kuna watoto hawana vyama, kuna vikongwe. Siku zote ni upendo na kuacha chuki. Aidha, Salma Kikwete hashindani na watu bali anatatua changamoto za wananchi,” alisema Mudhihir.