Vijana wa Dar es salaam Dances International (DDI) wakifanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi onyesho la kihistoria la kudansi lilotarajiwa kufanyika Katika Ukumbi wa Maonesho wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es salaam (picha na Mussa Khalid)
…………….
Tamasha la Museum Arts Explosion kwa kushirkiana na Dar es salaam Dances International (DDI) wameandaa onyesho Maalum la Kihistoria na kiutamaduni la kudansi linalotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa Sept 26 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa mazoezi ya kujiandaa kuelekea siku hiyo Kiongozi na Mwaasisi wa Kundi hilo Abdulkarim Juma maarufu Tayzdullah amewaomba watanzania kushiriki kwa wingi katika Maonesho hayo ili kuona Vijana wa kitanzania wakionyesha uwezo wao.
Aidha amewasisitiza Vijana kuepuka kukaa vijiweni badala yake watumie fursa ya kutumia vipaji vyao jambo litakalosaidia waweze kujikwamua kiuchumi na kuitangaza vyema Tanzania
“Tunawaomba wadau mbalimbali kushiriki siku hiyo kwani uwepo wao ni muhimu sana kwetu sisi kwa kjutuonyesha ushirikiano katika onyesho tunalolifanya’amesema Tayzdullah
Naye Choga Choga maarufu Dallazy amesema watu watakapojitokeza watashuhudia onyesho la kihistoria kwani wamekuwa wakifanya katika maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi.
Amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi ili waweze kujionea na kujifunza utamaduni kutoka kwa vijana hao katika onyesho lao watakalolifanya kwani litakuwa ni tukio kubwa la kisanaa.
Tamasha la Dar es Salaam Dances International, lililohuishwa na maonyesho ya kusisimua,na sanaa ya kustaajabisha wanashiriki wasanii mahiri kutoka pande mbalimbali ambapo hilo ni zaidi ya tukio la sherehe ya sanaa, utamaduni, na uvumbuzi lilotarajiwa kufanyika Katika Ukumbi wa Maonesho wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.