Askofu Mkuu wa kanisa la Baptist Tanzania, Dokta Anold Manasse akizungumza kwenye mahafali hayo jijini Arusha.
Meneja wa shule hiyo Lambert Hassan akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa darasa la saba katika shule ya mchepuo wa kiingireza ya Maromboso wakiimba kwenye mahafali hayo jijini Arusha.
……….
Happy Lazaro, Arusha
JAMII nchini imetakiwa kuhimiza swala.la maadili kwa watoto wao kwani mmonyoko wa maadili unaoendelea hivi sasa ni kutokana na wazazi kutosimamia nafasi zao ipasavyo.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Askofu Mkuu wa kanisa la Baptist Tanzania,Dokta Anold Manasse wakati akizungumza katika mahafali ya katika shule ya mchepuo wa kiingireza ya Maromboso iliyopo jijini Arusha .
Amesema kuwa ,kila mmoja wetu ana wajibu mkubwa wa kuhakikisha anafundisha maadili kwa watoto wetu kwani sisi ndio tunatakiwa kuwajengea misingi iliyo bora kwa maisha yao ya baadaye.
Askofu Manase amewataka wazazi pia kuhakikisha wanaombea nchi yetu katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao kwani sisi wenyewe ndio tuna wajibu mkubwa wa kuhakikisha tunatunza amani ya nchi yetu ili isiharibike hivyo kila mmoja apambane kwa nafasi yake.
Aidha amewataka wanafunzi wanaohitimu masomo yao nchini kuwa na bidii na kuhakikisha wanasikiliza wazazi wao kwani elimu pekee ndio itakayoamua wao wawe nani na wanataka kufika wapi kwa maisha yao ya baadaye
“Elimu pekee ndio itakayoamua na kuwasaidia mfike pale mlipokuwa mnataka kufika lazima mfikirie mnataka kuwa nani kesho mhakikishe mnaongeza bidii katika masomo yenu popote mtakapokuwa na hakikisha mnaachana na makundi yasiyofaa kwani yatawaharibia malengo yenu mliyojiwekea.”amesema .
Aidha amewataka wazazi pamoja na walezi kuhakikisha wanaendeleza ndoto za watoto wao kwani urithi pekee wa mtoto yoyote ni elimu na sio vinginevyo hivyo wahakikishe wanawekeza huko zaidi.
Meneja wa shule hiyo Lambert Hassan amesema kuwa shule hiyo imeendelea kufanya vizuri sana kutokana na elimu bora ambayo wamekuwa wakitoa kwa wanafunzi hao kwa kuzingatia maadili yaliyo.bora.
Amesema kuwa, shule.imeongeza kompyuta ili kumwezesha kila mwanafunzi kuweza kusoma somo hilo na hii ni kutokana na mabadiliko yanayoendelea sasa hivi ya sayansi na teknolojia .
Aidha amewataka wazazi pamoja na walezi kuhakikisha wanazingatia maadili ya watoto wao waliyofundishwa hapa shule pindi wanapokuwa majumbani na kuepukana na makundi yasiyofaa ambayo.mwisho wa siku yatawaharibia malengo yao.
“Wanafunzi nataka mtambue kuwa huu ni mwanzo tu ndo kwanza safari imeanza na naombeni sana mhakikishe mnayaendeleza yale yote mliyoyapata hapa shuleni na kuwa mabalozi wazuri wa kutangaza shule yetu.”amesema Lambert .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo,Mchungaji Goodluck Msumari amesema kuwa shule hiyo imekuwa ikiwaandaa watoto hao kwa ajili ya kesho yao kwa kuwafundisha kuweza kujitegemea zaidi badala ya kutegemea masomo ya darasani tu.
“Naombeni sana wanafunzi mnaohitimu leo mhakikisha mnaikamata sana elimu.msiiache iende zake maana huo ndio urithi pekee mliopewa na utakaowasaidia kwenye maisha yenu ya baadaye .”amesema