Klabu ya Simba SC imeanza kampeni yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gaborone United ya Botswana, katika mchezo wa hatua ya awali uliopigwa leo, Septemba 20, 2025, kwenye Uwanja wa Francistown, nchini Botswana.
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa katika dakika ya 15 na mshambuliaji Ellie Mpanzu, aliyeunganisha kwa kichwa krosi safi ya beki Shomari Kapombe akiwa ndani ya eneo la hatari.
Simba SC sasa inatarajiwa kurudiana na Gaborone United wiki ijayo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, ambapo mshindi wa jumla atafuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo mikubwa Barani Afrika.