Mgombea ubunge Jimbo la Sumbawanga mjini Aesh Halfan Hilary
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa Siraf Maufi wakati akiwaombea wagombea udiwani na ubunge kura
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni kusikiliza sera za mgombea wa chama cha mapinduzi CCM.
……………
Na Neema Mtuka Sumbawanga
Rukwa: Mgombea ubunge Jimbo la Sumbawanga mjini Aesh Halfan Hilary amesema endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa atahakikisha changamoto ya pembejeo za kilimo zinatatuliwa na wakulima kuondokana na changamoto hiyo.
Aesh akizungumza leo Septemba 15 wakati wa uzinduzi wa kampeni katika viwanja vya shule ya msingi Msua Manispaa ya Sumbawanga Mkoani hapa.
Aesh amesema wakulima wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa pembejeo za kilimo,na kukosa soko la kuuzia mazao yao.
“Mkinipa ridhaa nitahakikisha soko la kimataifa la mazao Kanondo linakamilika ili wakulima wakauze mazao yao pale tena kwa bei nzuri”.amesema Aesh.
Awali Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa Siraf Maufi akifungua mkutano huo wa kampeni amewaombea kura madiwani na
mgombea ubunge wa Jimbo hilo.
Baadhi ya wananchi akiwemo Richard Mtanga amesema kama endapo ahadi alizozitoa mgombea zitatkelezwa tutaondokana na changamoto kubwa ya kukosa mbolea ya ruzuku.
“Hatupati mbolea ya ruzuku kwa wakati ,na wakati mwingine hatupewi taarifa na hatimae unakuta msimu umekaribia na tunashindwa kulima kilimo cha kisasa kutokana na kukosa pembejeo za kilimo kwa sababu ya uzembe wa viongozi tulionao.”amesema Mtanga.



