Na Mwandishi wetu, Babati
TARINGIRE Pre & Primary English Medium School iliyopo mjini Babati Mkoani Manyara, imefanya mahafali yake ya saba mwaka 2025 kwa kuadhimisha kwenye hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Shule hiyo marufu na bunifu Mkoani Manyara ya mchepuo wa kingereza ya q Pre & Primary English Medium School iliyopo mjini Babati imefanya mahali yake ya darasa la saba mwaka 2025 kiubunifu zaidi tofauti na ukawaida unaofanyika mahali kwingine kwa kufanyika hifadhini.
Mahafali hiyo iliyokuwa inawaaga wanafunzi 40 waliofanya mtihani wa kumaliza darasa la saba iliyofanyika nchini kote Septemba 10 na 11 mwaka 2025 Ilifanyika kibunifu zaidi katika hifadhi ya Taifa ya Tarangire National Park iliopo Mkoani Manyara siku ya Jumamosi Septemba 13 mwaka 2025.
Mahafali hayo ya saba ya kiwango na bunifu yamehudhuriwa na wafanyakazi wote wa shule hiyo, wahitimu, wawakilishi wa wanaobaki na wawakilishi wa wazazi.
Mkuu wa shule hiyo Amos Temu akizungumza kwenye mahali hayo amesema shule ya Tarangire ina dhumuni kuu la kuleta dhamani endelevu (Sustainable Value) kwa wanafunzi, walimu, wazazi na wadau wake wote.
“Enendeni mkatekeleze kwa vitendo yale ambayo mlijifunza Tarangire School, kujiamini, ubunifu, juhudi katika Masomo, hofu ya Mungu, usafi wa maisha na jujiheshimu” amesema Temu.
Mmoja kati ya wahitimu hao Joan Wilberd Njau, ameushukuru uongozi wa shule hiyo akianza na meneja wa shule Bi Flora Ronald, walimu na wafanyakazi kwa kuleta mwamko mkubwa wa elimu katika mji wa Babati na Mkoa wa Manyara kwa ujumla.