Mgombea Ubunge wa jimbo la Kigoma mjini Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo) akipiga saluti akiwa juu yapikipiki katika maandamano kuelekea kwenye Mkutano mkubwa wa kampeni wa CCM kama Ishara ya Kuwashukuru wanaKigoma kwa kumuunga mkono na kumkaribisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye atawahutubia wananchi wa Kigoma mjini na kuwaomba kumpigia kura za ndiyo katika uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote.
Mkutano huo wa kampeni unafanyika viwanja vya Kutosho Bandari Kavu kata ya Fungu mjini Kigoma.
NA JOHN BUKUKU- KIGOMA