Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa Hali ya Hewa Tanzainia (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC) Dkt. Ladislaus Chang’a akizungumza na waandishi wa habari Leo Septemba 11, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akitoa maelekezo wa utabiri wa mvua za vuli.
……..
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa mvua za vuli ambapo mvua zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Chini ya Wastani katika maeneo mengi na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na kupunguza wa mvua hususani katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki.
Kupunguza huo wa mvua unatokana na uwepo wa kupungufu wa joto katika bahati ya Pasifiki.
Akizungumza na waandishi leo Septemba 11, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akitoa maelekezo wa mvua za vuli zinazotarajia kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba 2025, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC) Dkt. Ladislaus Chang’a, amesema kuwa mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Oktoba, 2025 katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.
Amesema kuwa mvua hizo zitasambaa katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba 2025. na kuisha mwezi Januari, 2026”.
“Mvua za Vuli zinatarajiwa kuongezeka kidogo mwezi Desemba, 2025 na Vipindi vya joto kali kuliko kawaida vinatarajiwa katika msimu huu wa Vuli” amesema Dkt. Chang’a.
Dkt. Chang’a amesema kuwa TMA imeendelea kutoa taarifa za utabiri wa msimu mahususi kwa ngazi ya Wilaya, ambapo Wilaya 86 zilizo katika ukanda unaopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka zitapatiwa utabiri huo wa maeneo madogo.
Msimu wa Mvua za Vuli ni mahususi kwa maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro), pwani ya kaskazini (kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, mikoa ya Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba), ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.
Dkt. Chang’a ametoa wito kwa wananchi kufuatilia taarifa za utabiri wa saa24, siku 10, mwezi na tahadhari zinazotolewa na TMA ikizingatiwa kuwa mwelekeo wa mvua uliotolewa ni kipindi cha msimu wa miezi mitatu.