Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania Bw. Shani Kinswaga (Kushoto) na Mkurugenzi wa GF Automobile Bw. Mujtaba Karmali (Kulia) wakisaini makubaliano ya ushirikiano katika ofisi za GF Automobile jijini Dar es Salaam tarehe 10 Septemba 2025. Hafla hiyo ilishuhudiwa na Mkuu wa kitengo cha sheria wa Benki ya Exim Tanzania Bw. Edmund Mwasaga na Mkuu wa Fedha za Shirika wa GF Automobile Bw. Raza Hussain Vakil. Ushirikiano huu utawezesha wateja wa Benki ya Exim kupata mikopo nafuu ya magari yenye masharti rahisi ya marejesho, hivyo kurahisisha safari ya umiliki wa magari kwa wateja binafsi na wafanyabiashara.
……………
Dar es Salaam, 10th September 2025 – Exim Bank Tanzania na GF Trucks & Automobile Limited wamesaini rasmi Mkataba wa Makubaliano (MoU), hatua inayoashiria ushirikiano uliobuniwa kurahisisha safari ya umiliki wa magari nchini Tanzania kwa kuwapatia wateja suluhisho la kifedha rahisi, nafuu na linalojikita katika mahitaji ya mteja.Hii ni njia ya kuthibitisha kwamba Exim inatoa zaidi ya huduma za kifedha kwa kuleta suluhisho linalorahisisha maisha ya kila siku.
Kupitia ushirikiano huu, wateja binafsi na wafanyabiashara wa Exim Bank wanaweza kumiliki magari mapya kabisa kwa kuchangia kiasi kidogo cha awali, huku wakinufaika na marejesho mepesi ya kila mwezi kwa muda wa hadi miaka sita.
Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Shani Kinswaga, “Hapa Exim Bank, wateja wetu ndio kiini cha kila kitu tunachofanya. Tumejizatiti kwenda mbali zaidi ya huduma za kifedha ili kurahisisha maisha ya wateja wetu. Kupitia ushirikiano huu na GF Automobile, umiliki wa gari unakuwa rahisi zaidi. Kuanzia upatikanaji wa mkopo, usajili hadi bima, kila kitu kinasimamiwa kwa urahisi ili mteja wetu aingie akiwa na hitaji na kutoka akiwa na suluhisho.”
Ushirikiano huu unaleta urahisi na uwazi katika mchakato mzima wa kupata gari. Wateja hawatalazimika tena kufuata mlolongo mrefu kwa sababu kila hatua ya mchakato utashughulikiwa na Exim pamoja na GF Trucks. Hii inamaanisha kuanzia upatikanaji wa mkopo, ukabidhi wa gari jipya yani zero kilomita, usajili na hadi bima vyote vinaunganishwa katika mfumo mmoja, na kufanya mchakato wa umiliki gari kuwa rahisi, nafuu na wenye uwazi kwa wateja.
Bw. Mujtaba Karmali, Mkurugenzi wa GF Automobile aliongezea: “Ushirikiano huu na Exim Bank ni fursa kubwa ya kuwasaidia Watanzania wanaotamani kumiliki magari lakini wanakwamishwa na changamoto za gharama za awali. Kupitia ushirikiano thabiti tumeweza kuwaletea wateja wetu bidhaa bora kupitia huduma ya mikopo kutoka Exim, tunafanya umiliki wa gari kuwa jambo la kweli kwa Watanzania wengi zaidi. Ushirikiano huu unawawezesha watu binafsi na biashara huku ukichochea ukuaji wa uchumi na kuwapa urahisi wa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine iwe kwa shughuli binafsi au za kibiashara “
Mbali na wateja binafsi, mpango huu utawezesha pia biashara ndogo, za kati pamoja na makampuni makubwa kupata magari ya kuendesha shughuli zao bila kuathiri biashara hizo. Kwa kuwezesha upatikanaji rahisi wa magari, ushirikiano huu unachochea shughuli za kiuchumi na kuongeza tija huku ukirahisisha ukuaji wa biashara.
Kwa upande wa Exim Bank, ushirikiano huu unathibitisha tena nafasi yake kama benki inayotoa zaidi ya huduma za kifedha kwa kutoa suluhisho linaloboresha maisha ya kila siku. Kwa GF Automobile, inayohusisha chapa kama Hyundai na Mahindra, mpango huu unapanua zaidi wigo wake wa soko kwa kutumia mtandao mpana wa wateja wa Exim Bank.
Kwa pamoja, taasisi hizi mbili zinashirikiana kwa lengo moja: kurahisisha umiliki wa magari kwa njia rahisi, yenye uwazi na endelevu. Kupitia utaalamu na rasilimali za Exim Bank na GF Automobile wanaweka kiwango kipya katika soko la magari Tanzania kwa kubadilisha umiliki wa gari kuwa rahisi na wenye ufanisi kwa kila mteja.
Wateja wanaweza kutembelea tawi lolote la Exim Bank au ofisi za GF Automobile nchini kote ili kuchunguza fursa za mikopo na kuanza safari yao ya umiliki wa gari leo.