Katika kijiji kimoja kilichopo pembezoni mwa mji wa Mwanza, aliishi mwanamke kijana aliyejulikana kwa jina la Mercy. Mercy alikuwa ameolewa na mume wake aitwaye Joseph kwa kipindi cha takribani miaka minne. Ndoa yao ilianza kwa furaha tele, lakini kadiri muda ulivyopita, changamoto moja kubwa ilianza kujitokeza—kutopata mtoto.
Katika jamii yao, mtoto huonekana kama nguzo ya ndoa na baraka ya kifamilia. Mercy alijaribu kwa kila njia kuhakikisha anapata ujauzito: alitembelea hospitali mbalimbali, alitumia dawa za hospitali, hata akajitahidi kuzingatia lishe bora kama alivyoelekezwa na madaktari. Lakini kila mara vipimo vilionyesha hali ya kawaida, jambo lililomchanganya sana….. SOMA ZAIDI