Na Mwandishi Wetu
ZANZIBAR, Septemba 8, 2025 – Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Ndugu Othman Masoud Othman, ameapishwa leo katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Kiapo hicho kilifanyika mbele ya Jaji Said H. Said huku kikishuhudiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mheshimiwa Khamis R. Abdallah.
Kwa mujibu wa taratibu, kiapo hiki ni sharti la kisheria kwa kila mgombea urais kabla ya kuanza rasmi mchakato wa kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ACT-Wazalendo pamoja na wadau wa siasa waliokuja kushuhudia tukio hilo muhimu kwa safari ya chama hicho kuelekea uchaguzi.