Dkt Nchimbi akizungumza na wanachama na wananchi wa Kalambo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya polisi kata ya Matai wilaya ya Kalambo.
Nchimbi katika ya viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi CCM
Dkt Nchimbi akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalambo Edfonce Kanoni
[9/8, 8:57 PM] Neemamtuka: Baadhi ya wananchi na wanachama waliojitokeza kusikiliza sera za chama cha mapinduzi.
………….
Rukwa: Mgombea mwenza wa urais,Balozi Dk.Emmanuel John Nchimbi amesema chama cha mapinduzi (CCM) itaisimamia serikali kumalizia uunganishaji wa umeme kwenye vitongoji vyote vilivyobakia.
Balozi Dkt Nchimbi amesema hayo leo Septemba 8 katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya polisi kata ya Matai wilaya ya Kalambo.
Akizungumza wilayani Kalambo Nchimbi amesema wataisimamia serikali kukamilisha mradi wa TAZA unaohusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha nchi za Tanzania na Zambia.
“Mradi huu pia utahusisha ujenzi wa vituo vya kupooza umeme katika wilaya ya Sumbawanga, Kalambo na Nkasi.” Amesema Nchimbi
Aidha Nchimbi amesema wataimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala na kuongeza upatikanaji wa gesi asilia katika viwanda,taasisi,Majumbani na kwenye magari.
Nchimbi amesisitiza kuwa chama kitaendelea kusimamia serikali kuhakikisha inakuza na kuwezesha shughuli za kiuchumi zinazoanzishwa na kuendeshwa na watanzania ili kuwapa fursa za kiuchumi.
Kesho Septemba 9 2025 Nchimbi atakuwa Sumbawanga mjini katika viwanja vya ofisi ya mtendaji wa kata ya majengo Manispaa ya Sumbawanga.